BREAKING NEWS -NAIROBI KENYA
WATU zaidi ya 100 wamekufa baada ya kuzuka moto kwenye bomba la mafuta lililopasuka karibu na kituo kimoja cha eneo la viwanda jijini Nairobi.
Inaaminika wengi wa waliokumbwa na mkasa huo walikuwa wakiiba mafuta.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Capital News, miili 102 ya watu ilikuwa imepatikana hadi mchana wa leo ambako kazi ya uokoaji ilikuwa ngumu kutokana na eneo lenyewe lilipo, na kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda moto huo ungeenea katika makazi ya watu waishio karibu.
0 comments:
Post a Comment